NEC YAKAMILISHA RASIMU YA KWANZA YA TARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA OCTOBA 2015

NEC YAKAMILISHA RASIMU YA KWANZA YA TARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA OCTOBA 2015

Like
344
0
Tuesday, 03 May 2016
Local News

KAMATI Maalumu iliyoundwa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika nchini Oktoba 25 mwaka 2015 imekamilisha Rasimu ya kwanza ya Taarifa hiyo na kuiwasilisha kwa Tume.

 

Akizungumza Katika kikao cha Tume baada ya kupokea Rasimu hiyo ya kwanza, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amepongeza kazi iliyofanywa na Kamati hiyo licha ya majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Tume hiyo kwa sasa.

 

Jaji Lubuva ameeleza kuwa Tume imeridhishwa na kazi iliyofanywa ya kuandaa Rasimu hiyo ikiwa ni pamoja na muda mfupi uliotumika katika kukamilisha kazi hiyo.

Comments are closed.