NEC YAWATAKA VIONGOZI WA SIASA KUEPUKA TAARIFA ZISIZO SAHIHI KUHUSU TUME HIYO

NEC YAWATAKA VIONGOZI WA SIASA KUEPUKA TAARIFA ZISIZO SAHIHI KUHUSU TUME HIYO

Like
201
0
Monday, 12 October 2015
Local News

TUME ya Taifa ya Uchaguzi-NEC, imewataka viongozi wa vyama vya siasa kuepuka kutoa taarifa na shutuma sisizo sahihi kuhusu Tume hiyo na badala yake wajikite katika kufikisha taarifa zilizo sahihi na zilizokusudiwa kwa Wafuasi wao na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba 2015.

 

Akizungumza leo katika  Mkutano wa Tume na viongozi  wa vyama vya siasa jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, amesema Tume imeaandaa vituo vya kupigia kura elfu 65,105 Tanzania Bara ni Vituo 63,525 na Zanzibar ni Vituo 1,580 ambapo amebainisha kuwa Kila kituo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia  Wapiga Kura  450 na wasiozidi 500.

Comments are closed.