NEPAL: NDEGE YA ABIRIA YATOWEKA

NEPAL: NDEGE YA ABIRIA YATOWEKA

Like
233
0
Wednesday, 24 February 2016
Global News

NDEGE ndogo iliyowabeba abiria 21 imetoweka ikiwa maeneo yenye milima nchini Nepal.

Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Pokhara, magharibi mwa mji mkuu Kathmandu, kwenda Jomsom, eneo ambalo watu wengi wanaoenda kukwea milima ya Himalaya huanza safari yao ya kukwea milima hiyo.

Hakuna viwanja vya ndege kati ya maeneo hayo mawili na inahofiwa kwamba ndege hiyo ya shirika la ndege la Tara Airlines imeanguka.

 

Comments are closed.