NEPAL YAPATA RAIS WA KWANZA MWANAMKE

NEPAL YAPATA RAIS WA KWANZA MWANAMKE

Like
354
0
Thursday, 29 October 2015
Global News

BUNGE la nchini Nepal limemchagua mtetezi wa haki za wanawake Bidhya Devi Bhandari kuwa rais wa kwanza mwanamke, katika hatua ambayo imetajwa kuwa ya kihistoria.

Mwanamke huyo wa miaka 54 kwa sasa ndiye Naibu mwenyekiti wa chama tawala cha kikomunisti ambaye awali alikuwa waziri wa ulinzi mwaka 2009 na 2011.

Bhandari atachukua nafasi ya Ram Baran Yadav, aliyekuwa rais wa kwanza wa Taifa hilo kuchaguliwa na watu mwaka 2008 baada ya Nepal kufuta utawala wa kifalme.

Comments are closed.