Nguo za kubana huathiri ‘mbegu za kiume

Nguo za kubana huathiri ‘mbegu za kiume

1
2067
0
Monday, 13 August 2018
Global News

Kuvaa nguo za ndani zilizo pana kunaweza kuwa njia rahisi kwa wanaume kuimarisha mbegu za kiume na homoni zinazozidhibiti, utafiti uliofanyika nchini Marekani umeeleza.

Utafiti uliowahusisha wanaume 656, uliofanywa na Chuo cha masuala ya afya cha Havard TH Cha nchini Marekani, wanaovaa boxer zilizo kubwa walikuwa na ongezeko kwa 25% ya ubora wa mbegu za kiume kuliko wanaume wanaovaa nguo za ndani zinazobana.

Kutokuwepo kwa hali ya joto kwenye maungo ya kiume kunaweza kuwa sababu.

Wataalamu wanasema mtindo huu rahisi wa maisha unaweza kuboresha uzazi wa wanaume

Uzalishaji wa mbegu za kiume haupendelei joto la zaidi ya nyuzi 34C, ndio maana korodani huning’nia kando ya mwili

Baadhi ya mitindo ya nguo za ndani, za kubana kama nguo za waendesha farasi, hubana maumbile hayo na kusababisha kutokea hali ya joto, huku mavazi ya ndani ambayo hayabani hufanya maumbile hayo kupata hewa ya kutosha.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *