NHIF YAJA NA MPANGO WA KUSAIDIA MATIBABU WANANCHI WASIOJIWEZA

NHIF YAJA NA MPANGO WA KUSAIDIA MATIBABU WANANCHI WASIOJIWEZA

Like
263
0
Wednesday, 18 February 2015
Local News

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya-NHIF umeanzisha mpango wa Kikoa ambao utatoa nafasi kwa Wananchi wasiokuwa na uwezo wa kuchangia gharama za Matibabu kutibiwa bure.

Wananchi wanaotarajiwa kunufaika na mpango huo ni kutoka katika Kaya masikini ambazo haziwezi kuchangia Shilingi 78,800 ambazo kila mwanachama anatakiwa kuchangia kwa mwaka.

NHIF imefikia uamuzi wa kuanzisha mpango huo ili kunusuru watu wengi wanaopoteza maisha kutokana na kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

Comments are closed.