Ni hatari kwa wanawake kufukiza  sehemu zao za siri.

Ni hatari kwa wanawake kufukiza sehemu zao za siri.

Like
1386
0
Friday, 09 August 2019
Global News

Madaktari wa magonjwa ya wanawake wameonya kuhusu hatari inayotokana na kutumia mvuke wa moto kwenye sehemu za siri, baada ya kutokea kuwa mwanamke mmoja alijiunguza sehemu zake za siri baada ya kutumia mvuke wa maji kufusha sehemu za siri.

Mwanamke huyo alikuwa na tatizo la kubadilika muundo wa maumbile ya sehemu zake za siri (prolapsed vagina) kitaalamu, na kuamini kuwa tiba hiyo itamfanya akwepe kufanyiwa upasuaji.

Kufusha kwa mvuke sehemu za siri, kitendo ambacho uhusisha kukaa kwenye chombo chenye maji ya moto chenye mchanganyiko wa maji na dawa, kimekuwa maarufu sana hivi sasa.

Tiba hiyo na tiba nyingine kwenye maeneo nyeti, imekuwa ikifanyika kwenye saluni na nyumba za Spa kwenye maeneo mbalimbali ya miji.

Nyumba za Spa zimekuwa zikitangaza kutoa huduma hiyo iitwayo ”v-steaming” ikidaiwa kuwa imekuwa maarufu miaka mingi barani Afrika na Asia. Wanasema tiba hiyo, ambayo wakati mwingine huitwa Yoni steaming hufanyika ”kuondoa uchafu” kwenye sehemu za siri.

Wataalamu hata hivyo, wanaasa kuwa ni hatari sana na hakuna uthibitisho wowote kisayansi kuwa ni tiba yenye kufanya kazi kiafya, ikiwemo kupunguza maumivu wakati wa hedhi au kusaidia kupata watoto.

Dokta Vanessa Mackay, msemaji wa shule ya wataalamu wa magonjwa ya wanawake, anasema ni ”imani” kuwa sehemu za siri zinahitaji usafi wa hali ya juu kiasi hicho au tiba ya namna hiyo.

Amesema inashauriwa kutumia sabuni zisizo na manukato kwenye eneo la nje la maungo hayo pekee.

”Sehemu za siri za mwanamke zina vijidudu vizuri, ambavyo husaidia kulinda maungo hayo,” alieleza katika taarifa yake.

Kuzifusha sehemu za siri kunaweza kuathiri vijidudu hivyo na kusababisha kuwashwa, na athari nyingine kama maumivu mithili ya kuwaka moto, pia ngozi laini pembezoni mwa sehemu za siri inaweza kuungua au kubabuka

Madaktari kadhaa wameeleza hadithi kuhusu mwanamke aliyepata madhara kutokana na kufusha sehemu zake.

Dokta Magali Robert, aliyeandika taarifa ya mwanamama huyo mwa miaka 60 wa huko Canada, alisema mwanamke huyo alijaribu kufukiza sehemu zake za siri kwa ushauri wa daktari wa tiba za kienyeji wa kichina.

Mwanamke huyo alikaa kwenye maji yaliyokuwa yamechemka kwa dakika 20 kwa siku mbili mfululizo kabla ya kujisalimisha kwa dharura baada ya kupata majeraha.

Alilazimika kuahirisha upasuaji ili kuuguza majeraha aliyoyapata.

Doka Robert anasema taarifa hizi za kupotosha huwafikia watu kwa wingi kwenye mitandao na taarifa kutoka kwa watu.

”Watu wanaotoa huduma kwa wanawake wanapaswa kufahamu tiba mbadala ili waweze kuepuka madhara.”Alieleza kwenye makala yake.

cc;BBCswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *