NICK CANNON: MARIAH CAREY ANAUZA NYUMBA BILA KUNISHIRIKISHA

NICK CANNON: MARIAH CAREY ANAUZA NYUMBA BILA KUNISHIRIKISHA

Like
315
0
Tuesday, 10 March 2015
Entertanment

Nick Cannon adai aliekuwa mkewe Mariah Carey hakumuhusisha na jambo lolote kwenye mjadala wa kuuza nyumba.

Nick ameeleza kuwa meneja wao anaehusika na mambo yote ya kibiashara ndie alikuwa kinara wa kuongoza hatua zote muhimu katika uuzwaji wa nyumba hiyo ya kifahali na kumuweka kizani kwa asilimia mia moja kwa kutomfahamisha chochote kwa mujibu wa Nick.

Kwa mujibu wa chombo cha kusimamia sheria Cannon amesema hakuidhinisha jumba hilo la kifahari kuuzwa kwa dola milioni 9 za kimarekani, nyumba ambayo Nick na Mariah Carey walikuwa wakiishi

Nick anaamini kuwa meneja wao Michael Kane alihusika kinagaubaga na watu wa Mariah Carey kwenye dili hilo na baadae yeye kufahamishwa kama mtu wa mwisho.

Nick amedai nyumba sio tatizo kwake hata ikiuzwa ila tatizo ni meneja huyo kushindwa kumshirikisha kwenye hatua muhimu pia namna ambavyo mapato yatagawanywa baada ya nyumba kuuzwa

Nick ameomba kusitishwa kuuzwa kwa nyumba hiyo

Comments are closed.