NIGERIA: JESHI LAPEWA MWEZI MMOJA KUISAMBARATISHA BOKO HARAM

NIGERIA: JESHI LAPEWA MWEZI MMOJA KUISAMBARATISHA BOKO HARAM

Like
333
0
Monday, 21 December 2015
Global News

MSEMAJI wa jeshi la Nigeria Kanali Sani Usman, amesema wanajeshi wake wamewauwa wapiaganaji 12 wa kundi la Boko Haram, na kukamata shehena ya silaha na risasi kutoka kwa kundi hilo, ambalo uasi wake wa miaka sita umegharimu maisha ya maelfu ya raia.

 

Usman amesema wanajeshi waliwaua washukiwa wa ugaidi wa Boko Haram waliokuwa wanazitesa jamii za maeneo ya Sabon Gari na Damboa, na kwamba miongoni mwa waliouawa ni kiongozi wa magaidi hao katika mji wa Bulayaga.

 

Rais Muhammadu Buhari amelipa jeshi muda wa hadi mwishoni mwa mwezi huu kuusambaratisha uasi wa Boko Haram, ambao umeuwa karibu watu elfu 17 na kuwalazimisha wengine milioni 2.6 kuyakimbia makaazi yao tangu mwaka 2009.

Comments are closed.