NIGERIA YAOMBA MKOPO WA DHARURA

NIGERIA YAOMBA MKOPO WA DHARURA

Like
308
0
Monday, 01 February 2016
Global News

NIGERIA imeomba mkopo wa dharura wa jumla ya dola bilioni tatu na nusu kutoka Benki ya Dunia ili kujaribu kuziba pengo kwenye bajeti yake.

Uchumi wa Nigeria umeathiriwa sana na kushuka kwa bei ya mafuta duniani.

Waziri wa fedha nchini humo Kemi Adeosun amesema amekuwa akifanya mazungumzo na maafisa wa Benki ya Dunia. Hata hivyo,

hatua ya Nigeria kuomba mkopo wa dharura inashangaza ikizingatiwa kwamba siku chache zilizopita Shirika la Fedha Duniani (IMF) lilisema haihitaji usaidizi wa kifedha.

Comments are closed.