OBAMA AMPA POLE KIKWETE

OBAMA AMPA POLE KIKWETE

Like
291
0
Tuesday, 25 November 2014
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amepokea salamu za pole kutoka kwa Rais wa Marekani  Barak Obama.

Katika salamu zake Rais Obama ameelezea kufurahishwa na taarifa kwamba Rais Kikwete anaendelea vyema kiafya baada ya kufanyiwa upasuaji kwa mafanikio na kuondoa tatizo la tezi dume alilokuwa nalo.

Katika salamu zake, Rais Obama amesema kuwa alipata heshima kufanya ziara rasmi nchini Tanzania mwaka 2013, na pia kumualika Rais Kikwete kwenye mkutano wa  Marekani na viongozi wa Afrika mwaka huu.

Comments are closed.