OBAMA APUUZIA ONYO LA NETANYAHU

OBAMA APUUZIA ONYO LA NETANYAHU

Like
258
0
Wednesday, 04 March 2015
Global News

RAIS Barack  Obama wa Marekani, ametupilia mbali onyo alilotoa waziri mkuu wa Israel kuhusu mpango wa Iran wa Nuclear katika hotuba yake tata kwa bunge la Marekani.

Rais  Obama amesema Benjamin Netanyahu alishindwa kutoa suluhisho mbadala kuhusu suala kuu la jinsi ya kuizuia Teheran kutengeza silaha za Nuclear.

Waziri Mkuu Netanyahu ambaye alialikwa kuhutubia bunge na viongozi wa chama cha Republican alishutumu mkataba uliowekwa kati ya mataifa ya magharibi na Iran na kudai kuwa ni hatari .

 

 

Comments are closed.