OBAMA AWASHUTUMU WAPINZANI WAKE

OBAMA AWASHUTUMU WAPINZANI WAKE

Like
210
0
Wednesday, 18 November 2015
Global News

RAIS Barack Obama  wa  Marekani ameshambulia kile alichokieleza  kuwa ni hofu ya kupita kiasi juu ya kitisho cha usalama kinachosababishwa  na  wakimbizi kutoka  Syria.

Katika hatua isiyokuwa ya kawaida Rais Obama amewashutumu  wapinzani  wake  kisiasa, kwa kuwaweka wajane  na  yatima  katika  kundi  la  wahalifu.

Hata hivyo Kupatikana kwa  hati  ya  kusafiria ya  Syria  karibu  na mwili wa mshambuliaji katika mashambulizi ya mjini Paris  kumezusha  hofu miongoni mwa wabunge wa Marekani na  magavana  kwamba  wapiganaji wa jihadi wanajichanganya pamoja na wakimbizi ili kuendelea na mashambulizi hayo.

 

Comments are closed.