OBAMA AZINDUA HATUA MUHIMU KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

OBAMA AZINDUA HATUA MUHIMU KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

Like
204
0
Tuesday, 04 August 2015
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama amezindua kile alichokiita hatua muhimu zaidi ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Katika uzinduzi huo Rais Obama amesema kizazi hiki ni cha mwisho chenye kushughulikia suala hilo na kwamba imeilazimu Marekani kuchukua hatua madhubuti za kutokomeza visababishi vya mabadiliko ya tabia nchi.

Obama amesisitiza hatua kali kuchukuliwa haraka kupunguza gesi ya ukaa inayotoka katika viwanda vilivyopo nchini humo kwa theluthi moja ifikiapo mwaka 2030.

Comments are closed.