RAIS BARACK OBAMA wa Marekani amesema kuna haja ya Mageuzi zaidi nchini Myanmar katika kuelekea kuipata Demokrasia.
Akizungumza katika mji mkuu wa nchi hiyo Yangon leo, Rais OBAMA amekosoa jinsi watu wa dini za walio wachache wanavyotendewa na pia hatua ya kumzuia kiongozi wa upinzani, AUNG SAN SUU KYI, kutogombea Urais.
SUU KYI aliyeachiwa huru miaka minne iliyopita baada ya kuwekwa kwenye kifungo cha nyumbani kwa takribani miongo miwili, sasa ni mjumbe katika Bunge la nchi hiyo, ingawa anashindwa kugombea Urais katika uchaguzi wa Rais wa mwaka ujao kutokana na kuzuiwa kikatiba.