PAPA AWASILI MAREKANI

PAPA AWASILI MAREKANI

Like
212
0
Wednesday, 23 September 2015
Global News

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Marekani kuanza ziara ambako pia atahudhuria kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, na kuzungumza katika kikao cha Congress ya Marekani, ambacho kinajumuisha Baraza la Wawakilishi na Baraza la Seneti.

Papa Francis mwenye umri wa miaka 78 alipokelewa na Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama katika uwanja wa ndege za kijeshi wa Andrews karibu na Washington DC.

Awali, katika ziara yake ya siku tatu nchini Cuba, Papa Francis aliwataka raia wa nchi hiyo kuyazingatia mapinduzi mapya ya upendo na huruma.

Comments are closed.