PAPA FRANCIS AHIMIZA UMOJA NA UWAZI

PAPA FRANCIS AHIMIZA UMOJA NA UWAZI

Like
239
0
Thursday, 26 November 2015
Global News
 
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ameanza ziara yake Afrika kwa kuhimiza umoja, uwazi, kuwathamini vijana na kuyatunza mazingira.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki aliwasili Nairobi jana majira ya saa kumi na nusu jioni na kukaribishwa kwa shangwe na viongozi wa kisiasa na kidini uwanja wa ndege.
Baada ya kuwasili, alielekea Ikulu ambako alipanda mti kisha kukutana na Rais Uhuru Kenyatta kabla ya kutoa hotuba yake ya kwanza, lakini awali akimkaribisha kutoa hotuba, Rais Kenyatta, alieleza umuhimu wa ziara ya kiongozi huyo wa kidini, akimkumbusha kwamba kesho ni siku ya mapumziko na siku ya kitaifa ya maombi Kenya.

Comments are closed.