PEGIDA LAONGEZA WAFUASI UJERUMANI

PEGIDA LAONGEZA WAFUASI UJERUMANI

Like
199
0
Tuesday, 27 October 2015
Global News

KUNDI  linalopinga  uhamiaji PEGIDA  limehamasisha  idadi kubwa  ya  watu  wanaoliunga  mkono  katika  mji  wa mashariki  nchini  Ujerumani  wa  Dresden kujiunga na kundi hilo.

Kwa  mujibu  wa  kundi huru la wanafunzi linalofanya utafiti la Durchgezält, mkutano  wa  PEGIDA ulihudhuriwa na  watu  kati  ya  Elfu kumi hadi Elfu kumi na mbili.

Lutz Bachmann, mmoja  kati  ya  waasisi  wa  kundi  hilo, alihutubia  hadhara  hiyo  na  kukosoa msimamo  wa serikali  ya  kansela  Angela  Merkel, akidai imechukua uamuzi wa  sera za  uhamiaji  bila  ya  kuwashauri wananchi.

Comments are closed.