POLISI ISRAEL WAPAMBANA NA VIJANA WA KIPALESTINA

POLISI ISRAEL WAPAMBANA NA VIJANA WA KIPALESTINA

Like
309
0
Wednesday, 05 November 2014
Global News

POLISI nchini  Israel  wamepambana  na  vijana  wa Kipalestina  waliokuwa  wakirusha  mawe ndani  ya  uwanja wa  msikiti  wa Al-Aqsa  leo  baada  ya  makundi  ya Wayahudi  wenye  msimamo  mkali  kutangaza  mipango ya  kuzuru  eneo  hilo  licha  ya  wiki  kadhaa  za  hali  ya wasi  wasi.

Ziara  hiyo  iliyopangwa  na  kundi  la Wayahudi  ikiwa  ni  pamoja  na  wanasiasa  wa  siasa  za kizalendo  zaidi ilikuwa  ifanyike  wiki  moja  baada   ya jaribio  la  mauaji  dhidi ya  mmoja  kati  ya  wanaharakati maarufu  lililofanywa  na  Mpalestina  aliyekuwa  na  silaha na  kusababisha  Israel  kulifunga  eneo  hilo, ambalo  ni takatifu  kwa  Wayahudi  na  Waislamu.

Ghasia  hizo zimezuka wakati  waandamanaji  waliporusha  mawe  na  vitu vinavyoripuka  baada  ya  polisi kufungua  lango  la Mughrabi  kwa  watu  hao  wanaotaka  kuzuru eneo  hilo.

Comments are closed.