POLISI KENYA WALINDA BARABARA MOMBASA

POLISI KENYA WALINDA BARABARA MOMBASA

Like
283
0
Friday, 21 November 2014
Global News

POLISI waliojihami wanaendelea kushika doria katika barabara za mji wa Mombasa Pwani ya Kenya hata baada ya maombi ya Ijumaa

Hii ni baada ya vurugu kati ya polisi hao na vijana baada ya kufanya msako katika baadhi ya misikiti mjini humo.

Misikiti ambayo ilifanyiwa msako ambako inaaminika mafunzo ya itikadi kali za kidini inafanyika, ni Swafaa na Minaa.

Polisi wanadai kuwa misikiti hiyo hutoa mafunzo ya itikadi kali ikilenga kuwaunga mkono wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia Al Shabaab.

 

Comments are closed.