POLISI WAMEINGILIA KATI MAANDAMONO YA CHAMA CHA CUF

POLISI WAMEINGILIA KATI MAANDAMONO YA CHAMA CHA CUF

Like
345
0
Tuesday, 27 January 2015
Local News

POLISI Mkoa wa Dar es salaam wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi na wafuasi wa chama cha Wananchi-CUF, waliokuwa wamekusanyika kwa maandamano kwa lengo la kukumbuka mauaji yaliyofanyika Januari 26 na 27 mwaka 2001 Zanzibar na Bara kupinga matokeo ya Uchaguzi wa mwaka 2010.

Polisi wamemuweka pia chini ya ulinzi mwenyekiti wa Chama cha Wananchi- CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na viongozi wengine wa chama hicho katika kituo cha Polisi Chang’ombe, jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Taarifa za awali, chama cha CUF kiliomba kibali cha polisi kufanya hivyo lakini maombi hayo yalichelewa kutolewa wakati tayari wafuasi wa chama hicho wakiwa wamejiandaa kwa maandamano.

Kwa Mujibu wa Profesa Lipumba taarifa za kuzuiwa kufanya maandamano hayo zimemfikia jana usiku, na hivyo alikuwa akifanya juhudi za kuyazuia lakini ilishindikana.

Kwa mujibu wa Chama cha CUF, Maandamano hayo yalitarajiwa kuanzia katika Viwanja vya Ofisi za chama hicho Temeke na kuishia katika viwanja vya Zakhem Mbagala ambapo Mwenyekiti wa chama hicho pamoja na Viongozi mbalimbali walitarajiwa kuongoza wafuasi wa chama hicho huku yakiwa na lengo pia la kuhimiza kufanyika kwa uchaguzi Huru na Haki, mwaka 2015.

Comments are closed.