PROGRAMU ENDELEVU YAANZISHWA KUTATUA MATATIZO YA UZAZI

PROGRAMU ENDELEVU YAANZISHWA KUTATUA MATATIZO YA UZAZI

Like
259
0
Friday, 25 September 2015
Local News

KATIKA Kuhakikisha suala zima la uzazi salama linazingatiwa nchini ili kudhibiti vifo vya kina mama na watoto ,Muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama Tanzania umeanzisha programu endelevu ya  kushirikisha wananchi katika kupaza sauti zao kuhusu matatizo mbalimbali ya afya  yanayowakumba kipindi cha uzazi na jinsi gani serikali na Asasi mbalimbali zisizo za Kiserikali zinaweza kutatua changamoto hizo.

Mratibu Taifa wa muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama Tanzania ROSE MLAY  amewaambia wandishi wa habari leo,  kuwa Taasisi imekuwa ikipita mikoa mbalimbali kuzungumza na wananchi kuhusu uzazi salama  na kugundua kuwa asilimia 50 ya wanawake wanajifungulia majumbani kutokana na ufinyu wa huduma za uzazi za dharura.

Comments are closed.