PSPF NA NHIF KUWAPATIA WANANCHI HUDUMA ZA AFYA KWA BEI NAFUU

PSPF NA NHIF KUWAPATIA WANANCHI HUDUMA ZA AFYA KWA BEI NAFUU

Like
541
0
Wednesday, 18 November 2015
Local News

KATIKA kuhakikisha wananchi wanapata huduma za Afya kwa bei nafuu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii-PSPF-pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya-NHIF-wamesaini mkataba wa kutoa huduma hizo kwa wanachama waliojiunga na  mpango wa uchangiaji wa hiari wa PSP.

 

Akizungumza na Wadau mbalimbali wa Afya Jijini Dar es Salaam leo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando amesema kuwa wanachama hao watachangia kiasi cha shilingi Elfu 76 na 800 kwa mwaka ambapo wataweza kupata huduma bora za afya katika hospitali zote zilizosajiriwa na NHI.

 

Amebainisha kuwa ndani ya serikali ya awamu ya tano yenye kauli mbiu isemayo ‘Hapa Kazi Tu’ watahakikisha kila mtanzania kupitia vikundi mbalimbali vya wajasiliamali anafikiwa na mfuko wa NHIF ili aweze kupata huduma za matibabu ambazo zitawawezesha kuimarisha Afya zao.

Comments are closed.