RAIA WAKIGENI WATAKIWA KUTOJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

RAIA WAKIGENI WATAKIWA KUTOJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Like
224
0
Friday, 03 July 2015
Local News

MKUU wa Mkoa wa Manyara dokta JOEL BENDERA amewataka raia wa nchi za kigeni wa mkoa huo kutojitokeza na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwani atakayebainika atamchukulia hatua kali za kisheria.

Mkoa huo unatarajia kufanya zoezi hilo la uandikishaji wa kutumia vifaa vya kielekrtoniki –BVR– kwa mwezi mmoja ambapo wapiga kura takribani laki saba na elfu hamsini wanatajia kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura la mkoa wa Manyara.

Dokta Bendera ameyasema hayo wakati alipokuwa akikagua utekelezaji wa zoezi la uandikishaji wa daftari hilo kwa wananchi wa wilaya ya Babati linaloendelea kwenye sehemu mbalimbali za wilaya hiyo.

Comments are closed.