IMEELEZWA kuwa rais mpya ajaye nchini Tanzania anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakikisha Tanzania inaendelea kubakia kuwa moja kwa kudumisha Umoja na Amani kwani Tanzania inatokana na muungano wa nchi mbili.
Kauli hiyo imetolewa na rais Jakaya Kikwete jijini Stockholm – Sweden ambapo alikuwa akiongea na watanzania waishio Sweden mara baada ya kuwasili na kuanza ziara ya kikazi ya siku 3, kuanzia tarehe 3 hadi 5 Juni, mwaka huu.
Watanzania mbalimbali walioko nchini Sweden kwa ajili ya shughuli za kikazi, kimasomo na ambao wanaishi nchini Sweden, walifika kumpokea na kumsalimia Rais Kikwete ambapo pia wamemsomea risala pamoja na kutaka kujua kuhusu haki yao ya kupiga kura katika uchaguzi Mkuu ujao.