RAIS KIKWETE ASISITIZA WAJIBU WA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA KUSIMAMIA CHANGAMOTO NA MAPUNGUFU KATIKA UJENZI WA BARABARA

RAIS KIKWETE ASISITIZA WAJIBU WA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA KUSIMAMIA CHANGAMOTO NA MAPUNGUFU KATIKA UJENZI WA BARABARA

Like
213
0
Tuesday, 25 August 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa Mikoa na Serikali za Mitaa kusimamia changamoto na mapungufu katika usimamizi wa ujenzi wa barabara nchini ili kuleta manufaa kwa wananchi.

Ameongeza kuwa ni wajibu wa ngazi hizo za uongozi kuhakikisha kuwa kazi za barabara hazifanyiki kwa viwango duni na kukomesha uwepo wa upendeleo katika uteuzi wa wakandarasi wa kazi za ujenzi wa barabara kinyume cha Sheria ya Manunuzi.

Rais Kikwete ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Nne wa Mwaka wa Maofisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Bodi ya Mfuko wa Barabara na Wadau wa Barabara za Mamlaka ya Serikali za Mitaa uliohudhuriwa na Wakuu wa Mikoa yote nchini na wilaya zote Jijini Arusha.

Comments are closed.