RAIS KIKWETE KUWASILI BERLIN LEO

RAIS KIKWETE KUWASILI BERLIN LEO

Like
251
0
Monday, 26 January 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete leo atawasili Mjini Berlin, Ujerumani ambako akitokea Riyadh, Saudi Arabia, ambako anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa –Gavi Alliance, ambako viongozi mbali mbali duniani watajadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea.

Baada ya kumaliza ziara yake Ujerumani, Rais Kikwete atakwenda Ufaransa ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ufaransa. Aidha, Rais Kikwete atafungua jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania katika Ufaransa na pia nyumba ya balozi.

Rais Kikwete pia baada ya kumaliza ziara zake za kikazi katika nchi za  Ujerumani na Ufaransa atakwenda Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika -AU.

 

Comments are closed.