RAIS KIKWETE KUZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA LEO

RAIS KIKWETE KUZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA LEO

Like
289
0
Monday, 03 August 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta Jakaya Mrisho Kikwete leo anazindua maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama Barabarani ambayo kitaifa yanafanyika kwenye viwanja vya Tangamano mkoani Tanga.

 

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula amesema tayari Rais Kikwete ameshawasili mkoani humo jana na kupokelewa na viongozi mbalimbali kwa ajili ya uzinduzi wa maadhimisho hayo.

 

Magalula amesema baada ya Rais Kikwete kumaliza uzinduzi wa maadhimisho hayo leo jioni atapata nafasi ya kuwaaga wananchi wa mkoa wa Tanga kwenye viwanja vya Mkwakwani.

Comments are closed.