RAIS MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA CAG

RAIS MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA CAG

Like
297
0
Tuesday, 29 March 2016
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa dokta John pombe Magufuli, jana amepokea taarifa ya ukaguzi wa hesabu za serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu Jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu Rais Magufuli amepokea taarifa hiyo yenye ripoti tano, ikiwa ni utaratibu wa kikatiba unaomtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kukabidhi kwa Rais taarifa ya ukaguzi kabla ya mwisho wa mwezi Machi.

Baada ya kupokea taarifa hiyo Rais Magufuli ataikabidhi mbele ya Bunge katika siku saba za mwanzo za kikao kijacho cha Bunge kitakachofanyika mjini Dodoma.

MAG2

Comments are closed.