RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA KIFO CHA RUBANI MUINGEREZA ALIYEUAWA NA MAJANGILI

RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA KIFO CHA RUBANI MUINGEREZA ALIYEUAWA NA MAJANGILI

Like
338
0
Monday, 01 February 2016
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Mmuungano wa Tanzania Dokta  John Pombe Magufuli amesema amesikitishwa na kitendo cha kuuawa kwa rubani Mwingereza aliyekuwa akisaidiana na maafisa wa Tanzania kupambana na ujangili.

Rubani wa helkopta Kapteni Roger Gower, alifariki baada ya majangili kuifyatulia risasi na kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha wakati alipoungana na askari wanyamapori waliokuwa wakikabiliana na majangili katika pori la akiba lililopo katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.

Askari mmoja wa Tanzania alijeruhiwa wakati wa tukio hilo ambapo pia Tembo watatu walipatikana wakiwa wameuawa. Dkt Magufuli ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha waliomuua rubani huyo wanakamatwa na wanafikishwa mikononi mwa vyombo vya sheria.

HEL3

HEL2

HEL

Comments are closed.