rais wa kwanza mwanamke Ethiopia

rais wa kwanza mwanamke Ethiopia

Like
957
0
Thursday, 25 October 2018
Global News

Wabunge nchini Ethiopia wamemchagua Sahle-Work Zewde kuwa rais wa kwanza mwanamke Ethiopia.

Bi Sahle-Work ni mwanadiplomasia mwenye uzoefu ambaye sasa amekuwa kiongozi wa kipekee mkuu mwanamke barani Afrika.

Kuchaguliwa kwake katika wadhifa huo kunajiri wiki moja baada waziri mkuu Abiy Ahmed kuliteua baraza la mawaziri ambapo nyadhifa nusu katika baraza hilo zimewaangukia wanawake.

Katika hotuba yake ya kukubali wadhifa huo, rais Sahle-Work amezungumza kuhusu umuhimu wa kudumisha amani, vyombo vya habari nchini vinaeleza.

Amechaguliwa baada ya kujiuzulu ghafla kwa kiongozi aliyekuwepo Mulatu Teshome.

Mkuu wa wafanyakazi katika ofisi ya waziri mkuu, Fitsum Arega, alituma ujumbe katika mtandao wa twitter kwamba uteuzi huo wa “kiongozi mkuu mwanamke haidhihirishi viwango vya miaka ijayo, lakini pia inafanya kuwa jambo la kawaida kwa wanawake kuwa waamuzi wakuu katika maisha ya umma”.

Sahle Work Zewde ni nani?

Rais Sahle-Work amewahi kuwa balozi wa Ethiopia nchini Senegal na Djibouti.

Ameshikilia nyadhifa kadhaa katika Umoja wa mataifa , ikiwemo mkuu wa kujenga amani katika Jamhuri ya Afrika ya kati.

Kabla ya kuwa rais wa Ethiopia, Bi Sahle-Work alikuwa mwakilishi wa UN katika Umoja wa Afrika

Kwa mujibu wa katiba ya Ethiopia , rais hana nguvu ikilinganishwa na wadhifa wa waziri mkuu ambaye yeye ndiye, aliye na nguvu za kisiasa nchini.

Wanawake walioongoza mataifa ya Afrika

Rais wa Liberia,Ellen Johnson Sirleaf, 72, alitajwa kama mmoja wa washindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2011.

Alichaguliwa kama Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika mwaka 2005 miaka miwili baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 14 Liberia.

Joyce Banda alichaguliwa kama Rais wa kwanza mwanamke Kusini mwa Afrika April 2012.

Akawa rais wa Malawi alipomrithi mtangulizi wake aliyefariki kutokana na mshtuko wa moyo.

Saara Kuugongelwa-Amadhila aliteuliwa waziri mkuu wa Namibia mnamo 2015, akiwa amewahi kuwa waziri wa fedha kwa miaka kadhaa.

Akiwa na mwanachama wa muda mrefu wa chama cha South West Africa People’s Organization (SWAPO), alikuwa uhamishoni Sierra Leona akiwa katika chama hicho akiwana umri wamiaka 13.

Baada ya kuhitimu katika chuo kikuu Marekani Bi Kuugongelwa alirudi Namibia na kufanya kazi kwa muda mfupi katika ofisi ya rais wa kwanza Sam Nujoma.

Kwa wepesi alimpandisha cheo kuongoza tume ya kitiafa ya mipango. Baada ya hapo alishikilia wadhifa wa waziri wa fedha tangu 2003 hadi alipopandishwa katika wadhifa wa waziri mkuu na rais Geingob.rs.

Ameenah Gurib-Fakim, aliwahi kuwa rais wa Mauritania kabla ya kujiuzulu kufuatia mzozo wa kifedha uliokuwa unamkabili.

Alituhumiwa kutumia kadi ya fedha aliyopewa na shirika la misaada kununua vitu vya kibinfasi vyenye thamani ya maelfu ya dola.

Bi Gurib-Fakim ni mwanasayansi tajika na mnamo 2015 alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa katika wadhifa wa rais wa Mauritius.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *