RAIS WA UKRAINE ASISITIZA USITISHAJI WA MAPIGANO BILA MASHARTI

RAIS WA UKRAINE ASISITIZA USITISHAJI WA MAPIGANO BILA MASHARTI

Like
225
0
Thursday, 12 February 2015
Global News

MAZUNGUMZO tete ya amani mjini Minsk kati ya viongozi wa Ukraine, Urusi, Ujerumani na Ufaransa yemendelea hadi leo, wakijadili mpango wa kukomesha mapigano ya miezi 10 nchini Ukraine.

Mwanzoni mwa mazungumzo hayo marefu, rais wa Ukraine Petro Poroshenko amesisitiza juu ya usitishaji mapigano usio na masharti yoyote.

Chanzo kilicho karibu na mazungumzo hayo kilisema viongozi hao walipanga kusaini taarifa ya pamoja inayotoa mwito wa kutekelezwa kwa mpango wa amani wa awali uliyosainiwa kati ya serikali ya Kiev na waasi mwezi Septemba.

Comments are closed.