RAIS WA ZAMANI WA BURUNDI BAGAZA AFARIKI DUNIA

RAIS WA ZAMANI WA BURUNDI BAGAZA AFARIKI DUNIA

Like
390
0
Wednesday, 04 May 2016
Global News

RAIS wa zamani wa Burundi Kanali Jean-Baptiste Bagaza amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Sainte Elisabeth mjini Brussels nchini Ubelgiji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mshauri wa rais wa Burundi Willy Nyamitwe kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter imeeleza kuwa Kanali Bagaza aliingia madarakani Novemba 1976 kupitia mapinduzi ya kijeshi.

Hata hivyo baadaye aliondolewa madarakani kupitia mapinduzi mengine yaliyoongozwa na binamu yake Meja Pierre Buyoya mwezi Septemba mwaka 1987.

Comments are closed.