Raisi wa Burundi afungua mashtaka dhidi ya televisheni

Raisi wa Burundi afungua mashtaka dhidi ya televisheni

Like
900
0
Friday, 25 January 2019
Global News

Mahakama mjini Paris , nchini Ufaransa imeanza kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza dhidi televisheni moja ya nchini Ufaransa,mwanasheria wa Ubeligiji na Mwandishi wa habari wa Burundi kwa makosa ya kuikashifu nchi yake na hadhi yake.

Rais Nkurunziza anadai kuwa televisheni hiyo ya Ufaransa miaka miwili iliyopita ilionyesha picha video za mauaji ya kimbari kwa madai kuwa chama tawala cha Burundi ndicho kilichohusika.

Mahakama ya mjini Parisi nchini Ufaransa imeanza kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza dhidi ya televisheni moja ya nchini ya Ufaransa,mwanasheria wa Ubeligiji na Mwandishi wa habari wa Burundi David Gakunzi .

Rais Nkurunziza anadai kuwa televisheni hiyo ya Ufaransa, miaka miwili iliyopita ilionyesha picha za video za mauaji ya watu wengi,na kudai kuwa chama tawala cha Burundi ndicho kilichotekeleza mauaji hayo.Rais Pieere Nkurunzia,anasema kuwa picha hizo za video zilizoonyeshwa na televisheni ya Ufaransa,channel 3,zinadai mauaji hayo ya watu wengi yalifanyika katika viunga vya makazi ya Rais Nkurunziza jambo linalokanushwa na ambalo kwa sasa limefikishwa mahakamani

Mwandishi wa BBC Prime Ndikumagenge amesema kuwa, rais Nkurunziza amekanusha vikali kwamba picha hizo wala si za ndani ya Burundi bali zinavyoonekana ni kama zilichukuliwa mahala Fulani katika nchi za Afrika Magharibi.

Televisheni hiyo ya Ufaransa Channel -3 ilizirusha picha hizo mwaka 2016,wakati wa uchaguzi mkuu wa Burundi, ulioandamana na vurugu.Video hizo katika matangazo kupitia televisheni ya France Channel 3, zilionyesha mauaji ya watu wengi,yanayodaiwa kutekelezwa na wafuasi wa rais Pieere Nkurunziza.Picha hizo za video zimepewa jina la Proof of acts of violence in Burundi”ikimaanisha ‘Ushahidi wa vitendo vya machafuko ya Burundi.

Ndani ya picha hizo pia ,baadhi ya watu wanaoonekana wakizungumza lugha ya Kihausa,lugha ambayo haiongelewi nchini Burundi.

Mshitakiwa Bernard Maingai ambaye ni mwanasheria, anatuhumiwa kwamba ndiye aliyepeleka video hiyo ili ichezwe katika Runinga na Mwandishi wa habari David Gakunzi yeye anashitakiwa na rais Nkurunziza kwa tuhuma za mahoajiano aliyoyafanya kwenye runinga akizungumzia picha hizo.

Serikali ya Burundi imekuwa ikipata vikwazo kutoka kwa jumuiya za kimataifa,kwa madai kukiuka haki za binadamu na kwamba chama tawala nchini humo kina kundi la vijana linaloitwa Imbonerakure.Hata hivyo serikali ya Burundi imekuwa ikipinga madai hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *