Redoine Faid: Mhalifu sugu akamatwa miezi 3 baada ya kutoroka jela akitumia helikopta Ufaransa

Redoine Faid: Mhalifu sugu akamatwa miezi 3 baada ya kutoroka jela akitumia helikopta Ufaransa

1
558
0
Wednesday, 03 October 2018
Global News

Redoine Faid, mhalifu sugu raia wa Ufaransa ambaye alitoroka jela akitumia helikopta iliyokuwa imetekwa nyara amekamatwa tena na polisi.

Mhalifu huyo aliyekuwa akitafutwa sana nchini Ufaransa, alishikwa kaskazini mwa Paris, akiwa na ndugu yake na wanaume wengine wawili kwa mujibu wa ripoti.

Faid, 46, amejiita kuwa shabiki wa filamu za uhalifu, ambazo anasema zimemfundisha jinsi ya kufanya uvamizi.

Kwanza alishikwa mwaka 1998 kwa wizi ya mabavu. Kutoroka kutoka jela mwezi Julai ilikuwa ndiyo mara ya pili amefanya hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *