SALVA KIIR NA RIEK MACHAR WAAFIKIANA MUUNDO WA SERIKALI YA MPITO

SALVA KIIR NA RIEK MACHAR WAAFIKIANA MUUNDO WA SERIKALI YA MPITO

Like
311
0
Friday, 08 January 2016
Global News

HATIMAYE, RAIS  wa  Sudan  Kusini Salva Kiir  na  kiongozi  wa  waasi Riek Machar  wamefikia  makubaliano  ambapo  pande  hizo mbili  zimekubaliana  kuhusiana  na  muundo  wa   serikali ya  mpito.

 

Kwa mujibu  wa  makubaliano  hayo, serikali  inaruhusiwa kuteua  mawaziri  16, ambapo  upande  wa waasi wanaruhusiwa  kuteua  mawaziri  10.

 

Serikali  ya  mpito  iliyokubaliwa  itakuwa  madarakani  kwa miaka 3  kabla  ya  uchaguzi  mpya  kufanyika. Sudan Kusini  imekumbwa  na  vita  vya  wenyewe  kwa  wenyewe ambavyo  vimesababisha  maelfu ya  watu  kuuwawa.

 

Comments are closed.