SATA AWEKWA KWENYE MAKAZI YA MILELE

SATA AWEKWA KWENYE MAKAZI YA MILELE

Like
544
0
Tuesday, 11 November 2014
Global News

RAIS wa Zambia MICHAEL SATA amezikwa leo mjini Lusaka baada ya mwili wake kuwekwa kwa muda wa Wiki Moja na wananchi kutoa heshima zao za mwisho.

Viongozi wa Kidini kutoka Makundi mbalimbali ya Waumini wamefanya Sala katika jengo la Bunge, katika tukio lililohudhuriwa na Wanadiplomasia, Wanasiasa , ikiwa ni pamoja na Rais wa kwanza wa nchi hiyo KENNETH KAUNDA na mtangulizi wa SATA RUPIAH BANDA.

Wananchi wametoa heshima zao za mwisho hadi siku ya Jumapili kwa kupita mbele ya Jeneza la Rais SATA aliyefariki akiwa na umri wa miaka 77, Oktoba 28 mjini London wakati akitibiwa kutokana na ugonjwa ambao haukutajwa.

SATA3

 

Comments are closed.