Sergei Skripal: Wanadiplomasia wa Urusi wazidi kufurushwa katika nchi mbalimbali

Sergei Skripal: Wanadiplomasia wa Urusi wazidi kufurushwa katika nchi mbalimbali

Like
392
0
Tuesday, 27 March 2018
Global News

Malcolm Turnbull, amesema matukio haya ni kutokana na tabia zisizokubalika za Urusi

Australia imekuwa nchi ya karibuni kufukuza wanadiplomasia wa Urusi kutoka nchini kwake kutokana na shambulio la jasusi wa zamani wa urusi nchini Uingereza Sergei Skripal na binti yake ambao wako katika hali mbaya kiafya.

Novichok: Sumu iliyotumiwa kumshambulia jasusi wa Urusi
Waziri mkuu Malcolm Turnbull amesema uamuzi huo unatokana na shambulio hatari la kutumia kemikali za neva zinazotengezwa na Urusi na zilitomiwa mara mwisho vita vya pili vya dunia.Idadi ya wanadiplomasia wa Urusi wanaofukuzwa inazidi kuongezeka, na hii ndio idadi kubwa kuwahi kutokea katika historia.
Zaidi ya nchi 20 zimeungana na umoja wa Ulaya kuwafukuza zaidi ya wanadiplomasia 100.

Donald Trump amesema Urusi inapaswa kuachana na tabia zake hatarishi kwa mataifa mengine

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson amesema hatua hiyo ya nchi nyingine kuungana na Uingereza ni matokeo ya tabia ya Urusi kuingilia nchi za watu.
”Ambacho kimesababisha nchi zote hizi kuungana na sisi, ni kutokana na vitu ambayo urusi imefanya, nchi nyingi ndani ya miaka kumi wameshuhudia kama sio jaribio la mauaji kufanyika nchini mwao basi wameingiliwa katika uchaguzi wao na mitandao yao, aina zote za tabia zisizo kubalika za Urusi,” alisema Johnson.
Seneta wa Urusi Andrey Klimov anasema kuwa hakuna ukweli wowote wa shutuma dhidi ya Urusi bali ni propaganda dhidi yao.

Iceland imetangaza pia itasimamisha mazungumzo na mamlaka za Urusi na viongozi wake hawatahudhuria michuano ya kombe la dunia mwezi wa sita.
Nani hudhibiti kemikali hatari zaidi duniani?
Mapema Uingereza ilisema kuwa hawatatuma mawaziri wake pamoja na familia ya Malkia kushiriki kombe la dunia.

Boris Johnson amesema Urusi inapaswa kujichunguza mara mbili mbili

Itakumbukwa kuwa mwaka 1986 rais wa Marekani Ronald Reagan aliwatimua wanadiplomasia 80 wa Urusi.
Na mwaka 2016 uongozi wa Barack Obama uliwafukuza wanadiplomasia 35 kutokana na kudukua chama cha Democratic.

Comments are closed.