SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA UJENZI WA BARABARA KWA KINGO CHA RAMI

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA UJENZI WA BARABARA KWA KINGO CHA RAMI

Like
281
0
Thursday, 28 January 2016
Local News

SERIKALI imeahidi kuendelea na ujenzi wa barabara katika maeneo tofauti nchini kwa kiwango cha lami ili kutatua adha kubwa ya ubovu wa barabara ulipo katika maeneo mengi nchini.

 

Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Mhandisi Godwin Ngonyani wakati akijibu maswali ya wabunge waliouliza kuhusu mpango wa serikali kuboresha barabara zilizopo.

 

Akijibu swali la Mhe Richard Mganga Ndassa Mbunge wa Sumve (CCM) Mhandisi Godwin Ngonyani amesema katika mwaka wa fedha 2014/2015 na 2015/2016 serikali ilitenga jumla ya shilling millioni 200 kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 70 na taratibu za kumtafuta Mhandisi Mshauri zinaendelea.

Comments are closed.