SERIKALI YAANDAA MPANGO WA KUHIFADHI CHAKULA

SERIKALI YAANDAA MPANGO WA KUHIFADHI CHAKULA

Like
269
0
Tuesday, 20 January 2015
Local News

SERIKALI kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula- NFRA, imeandaa mpango wa utekelezaji wa muda mfupi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula kutoka tani laki moja na sitini elfu hadi kufikia tani laki nne katika kipindi cha mwaka 2016 na 2017.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa huduma za biashara wa NFRA, Mikalu Mapunda wakati  akizungumza na Kituo hiki kuhusu hali ya utunzaji wa chakula kanda zote zilizopo nchini.

Akizungumzia hali ya chakula cha ziada katika kipindi kilichopita, Mapunda amesema kuwa hadi kufikia mwaka huu, kuna ziada ya tani milioni moja kutoka tani laki 3 kwa mwaka jana.

 

 

Comments are closed.