SERIKALI YAANZA KUPITIA RIPOTI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU WANAFUNZI WANAOPATA MIMBA SHULENI

SERIKALI YAANZA KUPITIA RIPOTI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU WANAFUNZI WANAOPATA MIMBA SHULENI

Like
351
0
Friday, 30 January 2015
Local News

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imeanza kupitia ripoti ya wadau wa Elimu kuhusu tafiti za watoto wanaopata ujauzito wakiwa shuleni ili kuwawezesha watoto hao kupata elimu.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Mratibu wa Elimu Kitengo cha Jinsia kutoka Wizara ya Elimu, Chimpaye Marandu wakati wakijadili ripoti iliyowasilishwa na Taasisi ya Policy Forum kuhusu tatizo la mimba kwa wanafunzi.

Marandu amesema kuna idadi kubwa ya watoto wa kike wanaokosa Elimu kwa sababu ya kupata ujauzito, na kwamba ripoti hiyo imeonyesha changamoto nyingi wanazozipata wanafunzi wa kike hali inayopelekea kupata ujauzito ikiwemo usafiri, umbali wa shule na uhaba wa Mabweni.

 

Comments are closed.