SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeipa hadhi ya kuwa Hospitali Wilaya iliyokuwa Zahanati ya Msoga ambayo tayari imekamilisha jengo lake jipya la Hospitali hiyo inayotarajia kuanza kazi Mwezi Aprili mwaka huu.
Akitoa maagizo hayo baada ya ukaguzi wa timu ya wataalam kutoka Wizara hiyo ya Afya , Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla waliofanya hivi karibuni katika Hospitali hiyo, ameeleza kuwa kuanzia Mwezi Aprili itaanza kazi kwa kuanza na huduma za wagonjwa wa nje na baada ya miezi mitatu itaendeshwa na huduma zote muhimu ikiwemo kulaza wagonjwa.
Majengo ya Hospitali hiyo yapo katika Kituo cha afya cha Msoga, kata ya Msoga, Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani, Ni miongoni mwa Hospitali itakayokuwa ya kisasa na kubwa.
Jengo hilo la Hospitali ya Wilaya inavyoonekana kwa nje