SERIKALI YAKEMEA TABIA YA KUSHAMBULIA WATUMISHI WA AFYA

SERIKALI YAKEMEA TABIA YA KUSHAMBULIA WATUMISHI WA AFYA

Like
259
0
Thursday, 31 March 2016
Local News

SERIKALI imekemea tabia inayotaka kujengeka ndani ya jamii ya kuwashambulia watumishi wa afya hasa Madaktari na Wauguzi.

Kufuatia hatua hiyo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, mheshimiwa Ummy Mwalimu amevitaka vyombo ya dola kuwachukulia hatua wananchi wanaojihusisha na vitendo hivyo ambavyo vitaathiri utoaji wa huduma za afya kwa wananchi hasa wa kipato cha chini.

Amewaonya wananchi kutoitumia vibaya dhamira ya dhati ya Rais Dkt. John Magufuli na Serikali ya kuimarisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma kwa kujichukulia sheria mkononi.

Comments are closed.