SERIKALI YATAKIWA KUREJESHA MAZUNGUMZO YA MAHAKAMA YA KADHI

SERIKALI YATAKIWA KUREJESHA MAZUNGUMZO YA MAHAKAMA YA KADHI

Like
211
0
Tuesday, 07 April 2015
Local News

Kutokana na Sesrikali kushindwa  kutoa tamko dhidi ya Muswada wa Mahakama ya Kadhi, Jumuiya ya Waislam na Taasisi 11 za Waislam, wameitaka Serikali kuonesha dhamira ya dhati kwa kurejesha mchakato wa mazungumzo baina yake na Waislam  juu ya suala hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Sheikh MUSSA KUNDECHA,  amesema kuwa ,Serikali imeshindwa kutoa tamko kamili na badala yake Makanisa na Viongozi wa dini ndiyo wamekuwa wakitoa tamko juu ya Mahakama hiyo.

Comments are closed.