POLISI mjini Damaturu, Nigeria, imesema Mshambuliaji wa Kike wa kujitoa Mhanga amejilipua katika Kituo kimoja cha Basi kilichokuwa kimejaa watu mjini humo na kusababisha vifo vya watu 16 huku wengine zaidi ya 30 wakijeruhiwa.
Mji wa Damaturu ulioko Kaskazini Mashariki mwa Nigeria umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa Boko Haram.
Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo amesema amesema amesikia mlipuko uliosababisha taharuki katika eneo hilo.