SHERIA YA MTOTO YA MWAKA 1971 YACHANGIA UWEPO WA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI

SHERIA YA MTOTO YA MWAKA 1971 YACHANGIA UWEPO WA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI

Like
296
0
Friday, 05 June 2015
Local News

SEREKALI  imetakiwa kuangalia upya sheria ya  mtoto ya mwaka 1971
kwani imebainika kuwa ni chanzo kimojawapo kinachoruhusu uwepo wa
ndoa na mimba za utotoni.

 

Akizungumza katika kongamano lililoandaliwa na shirika la
intiative for youth –INFOY– mwenyekiti wa baraza la watoto wilaya
ya Arusha HASSANI OMARY amesema kuwa ni wajibu wa serekali kuangalia
upya sherika hiyo kwani imekuwa ikiwaathiri watoto wengi
hapa nchini.

 

Amesema kuwa sheria hii imekuwa ikiruhusu watoto hata wenye umri chini
ya miaka 18 kuolewa  iwapo tu wazazi wake watakapo kubali kitu ambacho
kinawaathiri watoto wengi katika masomo yao na kimaisha kwa ujumla.

Comments are closed.