SHIRIKISHO LA VYUO VIKUU CCM LAMPONGEZA MAGUFULI

SHIRIKISHO LA VYUO VIKUU CCM LAMPONGEZA MAGUFULI

Like
369
0
Tuesday, 03 November 2015
Local News

SHIRIKISHO la Vyuo vikuu la Chama cha mapinduzi-CCM-limempongeza Rais mteule wa Jamhuri  Ya Muungano wa Tanzania dokta John Pombe Magufuli kwa kushinda kiti cha Rais, ikiwa ni kielelezo cha utendaji bora aliouonyesha katika kuwatumikia watanzania kupitia nafasi alizopitia kabla ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa shirikisho hilo Bi Zainab Abdallah amesema kuwa Rais Mteule Dokta Magufuli ndiye mtu pekee ambaye watanzania walikuwa wanamuhitaji ili aweze kuwaletea maendeleo kupitia uchapa kazi wake.

 

Aidha amesema kuwa Rais Mteule ameonesha dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo watanzania hivyo ni wajibu kwa kila mtu kusisitiza umoja na kuondoa tofauti zilizopo ili kujenga uchumi wa taifa.

Comments are closed.