SERIKALI ya Sierra Leone imesema italipa dola elfu tano za kimarekani kama fidia kwa familia ya kila mfanyakazi wa afya ambaye amefariki baada ya kuambukizwa Ebola wakati akihudumia wagonjwa wa Ebola.
Kituo cha taifa cha kupambana na Ebola nchini humo kimesema fidia hiyo ya mara moja pia itatolewa kwa ndugu wa wafanyakazi wa afya zaidi mia moja ambao wamekufa kwa ugonjwa huo hapo awali.
Virusi vya ugonjwa huo vimekuwa vikisambaa kwa kasi nchini Sierra Leone ambapo katika muda wa siku tatu zilizopita zaidi ya watu mia tatu wamegundulika kuambukizwa ugonjwa huo.