Soko la Facebook latetereka kwa kupoteza uaminifu

Soko la Facebook latetereka kwa kupoteza uaminifu

Like
543
0
Sunday, 25 March 2018
Global News

Pamoja na mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerbag kuomba msamaha kutokana na kupoteza uaminifu kitu kilichowakera watu zaidi ya milioni 50 duniani, soko lake la hisa limeonyesha kutetereka.
Kwa mujibu wa mtandao wa kibiashara MoneyWatch soko la hisa za mtandao huo zilianguka kwa asilimia saba.

Thamani ya hisa ilishuka kutoka Dola 176.80 siku ya Jumatatu hadi Dola 159.30 siku ya Ijumaa jioni.

Siku hiyo hisa za mtandao wa Facebook ziliuzwa kwa $38 kila moja na kuufanya mtandao huo kuwa na thamani ya kibiashara ya Dola bilioni 104.

Hadi Februari 2018 kutokana na kukua kwa matangazo ya kidijitali hisa za facebook zilipanda hadi $190.

Mchambuzi wa masuala ya hisa Raymond James amesema katika ripoti kwa wateja wake kwamba kumekuwa na ongezeko la wasiwasi juu ya Rashia kuendelea kuwalenga wateja na kutumia vibaya taarifa zao kitu ambacho kimekuwa na athari hasi katika hisa za Facebook.

Facebook imesema kuwa hapo awali ilitoa taarifa za wateja wake kwa mtafiti ambaye alidai kuwa zitatumika kwa masuala ya kielimu. Facebook imedai kuwa mtafiti huyo baada ya hapo “alitudanganya” na kuwapa taarifa hizo kampuni ya Cambridge Analytica.

Hali kadhalika Cambridge Analytica inashutumiwa kwamba ilihusika kwenye mzozo wa kupotosha watu na kutumia takwimu visivyo, ambao pia unaikabili kampuni ya Facebook.

Facebook tayari imesitisha uhusiano wake na CA na kuikataza kampuni hiyo kutumia mtandao huo kwa matangazo yake.

Hili lilikuwa ni tatizo kubwa la kupoteza uaminifu. Ninaomba msamaha wa kweli kwa kilichotokea. Tunawajibu wa msingi kulinda taarifa za watu,” Zuckerbag aliliambia shirika la habari la CNN.

Hata hivyo mmiliki huyo wa Facebook hakufafanua ni makosa gani Facebook ilifanya, lakini aliahidi kupitia apps zote na kuzihakiki kikamilifu iwapo zimehusika na vitendo vya jinai.

Wachambuzi wa biashara wanasema kuwa siri ya mafanikio ya modeli ya biashara ya Facebook ni kiwango cha wateja wanaojiunga na facebook, na hivi sasa kutokana na kashfa ya kupoteza uaminifu wake, Facebook imeanza kupoteza wateja wake.

Comments are closed.