SOMALIA: WANAJESHI WA KENYA WALIPEWA TAHADHARI

SOMALIA: WANAJESHI WA KENYA WALIPEWA TAHADHARI

Like
277
0
Friday, 22 January 2016
Global News

IMEELEZWA kuwa Wanajeshi wa Kenya nchini Somalia walionywa kuhusu shambulizi la kundi la Alshabaab siku 45 kabla ya kundi hilo kuvamia mojawapo ya kambi zao.

Jenerali Abas Ibrahim Guery ameiambia BBC kuwa , Kenya ilipewa ripoti ya kiintelijensia kuhusu tishio la uvamizi huo ambapo Wapiganaji hao wa kiislamu wanasema kuwa waliwaua zaidi ya wanajeshi 100 katika shambulio hilo likiwa ni baya zaidi kuwahi kufanyika kwa jeshi la Kenya.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewatambelea baadhi ya wanajeshi waliojeruhiwa katika hospitali ya Jeshi iliopo Nairobi kabla ya kuhudhuria hafla ya kuwakumbuka wanajeshi hao.

Comments are closed.